Neno la Shukrani na Ukaribisho
Katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu โ Amina.
Napenda kumshukuru Mungu wetu aliye hai kwa upendo na neema yake kuu inayotuwezesha kuendelea kushuhudia Injili ya Yesu Kristo katika maisha yetu ya kila siku. Ni furaha kubwa kwetu, kama Usharika wa KKKT Geza Ulole โ Kigamboni, Dar es Salaam, kuweza kuwa na ukurasa huu wa mtandaoni kwa ajili ya kuungana na waamini wote popote walipo.
Kwa niaba ya wachungaji wenzangu, viongozi, na waumini wote wa Usharika, ninawakaribisha kwa moyo wa upendo kutembelea tovuti hii ili kupata taarifa mbalimbali za huduma zetu, mafundisho, na matukio ya kanisa. Tunatamani ukurasa huu uwe daraja la kuwaletea neno la Mungu, nafasi ya kushiriki pamoja, na kujengeana imani thabiti katika Kristo.
Karibuni nyote โ tushirikiane, tupendane, na tumtumikie Bwana kwa moyo mmoja. Mungu awabariki sana.
Mchungaji Kiongozi
KKKT Usharika wa Geza Ulole โ Kigamboni,
Dar es Salaam.